Maelfu ya Wandamanaji wa Sri Lanka Wavamia Ikulu Kupinga Ugumu wa Maisha



Maelfu ya Waandamanaji wakiwa nje ya Ikulu ya Rais wa Sri Lanka, Gotabaya Rajapaksa.

MAELFU ya waandamanaji wamevamia makazi ya Rais Gotabaya Rajapaksa katika mji mkuu wa  Sri Lanka waandamanaji kutoka maeneo yote ya nchi waliandamana hadi mjini Colombo kudai kujiuzuru kwake baada ya maandamano ya miezi kadhaa kuhuusu kushindwa kudhibiti mzozo wa kiuchumi unaoikumba nchi hiyo.

Taarifa zinasema kuwa Rais alikuwa ameondolewa tayari na kupelekwa katika eneo salama wakati waandamanaji waipoingia nyumbani kwake.

Nchi hiyo inakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa na inahangaika kuagiza chakula, mafuta na madawa.

Maelefu ya waandamanaji wanaoipinga serikali walisafiri hadi katika mji mkuu, huku maafisa wakiliambia shirika la habari la AFP kwamba wengine hata ‘’waliziamrisha’’ treni kufika pale Polisi walifyatua risasi angani na kutumia gesi za kutoa machozi kuzuia umati wa watu kuingia.

“Rais alikuwa akisindikizwa kumepekwa mahali salama,” afisa wa ngazi ya juu wa ulinzi aliiambia AFP maafisa walijaribu kuwazuia waandamanaji kwa amri ya kutoka nje lakini walilazimika kuiondoa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad