Winga huyo wa klabu ya Manchester City ambaye kwa sasa analipwa kwa euro mil 120,000 sawa na Tsh 281,954,557/= kwa wiki Riyad Mahrez ametania kuwa hangeweza kumudu kutengeneza simu yake iliyoharibika hadi asaini mkataba mpya Manchester City.
Winga huyo wa Algeria ameongeza muda wa kukaa Etihad hadi 2025, baada ya kuingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa awali mwanzoni mwa mwezi huu.
Baada ya kukubali kufanyiwa marekebisho ya mkataba alikibali kusaini na alikuwa sehemu ya kikosi cha City kilichoondoka Jumamosi asubuhi kuelekea Marekani kwa ziara ya maandalizi ya msimu mpya.
wakati waondoka kuelkea Marekani Mahrez Alipost picha kwenye Twitter akiingia kwenye ndege, lakini wafuasi waligundua haraka kuwa alikuwa ameshika simu iliyopasuka.
‘Mahrez una pesa,’ shabiki mmoja alijibu, huku wengine wengi wakishangaa kwamba mchezaji wa Ligi ya Premia anaonekana kushindwa kurekebisha simu yake.
Lakini kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 alitoa jibu la kufurahisha. “Nilikuwa nikisubiri mkataba mpya,” alitania.
Mahrez alijiunga na City kutoka Leicester kwa pauni milioni 60 mwaka 2018 na amefunga mabao 63 katika mechi 189 alizochezea klabu hiyo.
Ameshinda Ligi ya Premia mara tatu chini ya uongozi wa Pep Guardiola – akiongeza taji moja alilonyanyua akiwa na Foxes msimu wa 2015-16 – na pia ameshinda Vikombe vitatu vya Carabao na Kombe moja la FA.