WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemueleza Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum kwamba dua aliyomuombea ili aoe mke wa pili ni dua isyokubalika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo tarehe 2 Julai, 2022 wakati akihutubia kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya duniani yanayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
“Sheikh Alhad aliomba dua isiyokubali, nataka nimwambie wazee muda huu kule Peramiho wapo kanisani kupinga dua yako isikubalike,” amesema Majaliwa na kufanya umati uliohudhuria maadhimisho hayo kuangua kicheko.
Katika ufunguzi wa maadhimisho hayo, Sheikh Alhad amemuombea Waziri Mkuu aoe mke wa pili ilia pate utulivu zaidi katika mizunguko yake.
Katika dua hiyo ya ufunguzi Sheikh Alhad ameswali hivi; “Tunamuombea sana Waziri mkuu ambaye ndiye mgeni rasmi wa jambo hili, tumeshuhudia hasa sisi viongozi wa dini namna ambavyo na akijituma kwa ajili ya watanzania.
“Suala la sana suala la Ngorongoro, Loliondo… Waziri mkuu ammewathibitishia Watanzania kwamba serikali ina nia njema na raia wake na hakuna raia ambaye atakosa haki au kunyanyaswa kwa namna yoyote ile, amekuwa halali hapumziki.
“Tunamuombea Mwenyezi Mungu aendelee kumbariki Majaliwa Kassim Majaliwa na ikikupendeza aongeze pia mke wa pili aweze kupata utulivu zaidi katika mizunguko yake,” Sheikh Alhad Mussa Salum.
Waziri ameoa mke mmoja pekee anayefahamika kwa jina la Marry Majaliwa.