Majaribio ya VAR Kuanza Kutumika Leo Nusu Fainali Ligi ya Vijana




Teknolojia ya Usaidizi wa marejeo ya picha za mnato kwa Waamuzi ‘VAR’ inataraji kutumika leo Ijumaa, Julai 15, 2022 kwa majaribio kwenye michezo ya Nusu Fainali ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya miaka 20 nchini Tanzania.

“Kwa mara ya kwanza, kwa maana ya mashindano, kwa maana kama nchi tunakwenda kufanya majaribio ya VAR katika michezo ya nusu fainali kwa maana ya kwamba Coastal Union na Mbeya Kwanza lakini pia Mtibwa Sugar na Azam”

“Kwahiyo ndani ya Uwanja wa Azam Complex Chamazi hizo set-up zitakuwa zimefanyika. Na patapokuwa na controversial zinazohitaji kufanyiwa hakiki kabla ya tukio, basi mwamuzi atapata nafasi ya kwenda kujiridhisha kabla ya kufanya maamuzi yake ya mwisho,” amesema Meneja wa Mashindano TFF – Baraka Kizuguto.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad