Wanafunzi 7 kati ya 17 waliojeruhiwa katika ajaili ya basi la Shule ya Msingi ya King David iliyotokea Julai 26, 2022 Mkoani Mtwara, wamepewa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam na wengine Hospitali ya Rufaa Ndanda, wilayani Masasi kwa matibabu zaidi.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Dkt. Clemence Haule amesema majeruhi wengine 10 waliobaki katika hospitali hiyo wanaendelea vizuri.
Tuju: Ruto alilipwa kumshika Uhuru
“Mgonjwa aliyeondoka jana alipata shida ya shingo na kuvunjika miguu ambapo leo asubuhi wawili wameenda pia Muhumbili na wawili wanaenda leo Ndanda kwa matibabu zaidi,” amesema Dk Haule.
Hapo jana baada ya kuaga miili ya merehemu na wazazi kukabidhiwa miili ya watoto wao, Mganga mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi aliwatembelea majeruhi ambao walikuwa katika hospitali na Ligulaili kuwajulia hali na kutoa pole kwa niaba ya Serikali.
Ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 13, kati yao ni wananfunzi 11 wa shule hiyo, na wawili ni dereva wa gari hilo aina ya Toyota Hince na mwanamke mmoja ambae alikua msaidizi wa wanafunzi ndani ya gari.