Makata, Naftari Wapunguziwa Adhabu ya Kifungo



ALIYEKUWA kocha wa Mbeya Kwanza, Mbwana Makata na meneja wa timu hiyo David Naftari wamepunguziwa ashabu yao ya kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitano na sasa itakuwa kwa miezi sita pekee.

Wawili hao awali walifungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitano kutokana na kosa la kukiuka sheria na kushinikiza timu yao kutocheza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Namungo iliyokuwa imepangwa kupigwa Mei 14 mwaka ambayo haikuchezwa.

Katika taarifa ya kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyotoka leo ikizingatia kikao chake cha Julai 6, imeeleza Makata na Naftari wamepunguziwa adhabu kutokana na wawili hao kukiri makosa yao na kuomba radhi.

“Makata na Naftari sasa watatumikia adhabu ya kufungiwa kwa muda wa miezi sita badala ya miaka mitano iliyotangazwa hapo awali".


Adhabu ya kufungiwa miezi sita imehesabiwa tangu siku ilipotangazwa adhabu ya kufungiwa miaka mitano, Mei 16, 2022.” Imeeleza taarifa hiyo.

Kwa mantiki hiyo, Makata na Naftari watakuwa tayari kujihusisha na soka kuanzia Novemba 16 mwaka huu.

Mbeya Kwanza waliyokuwa wakiitumikia wawili hao, ilishuka daraja msimu uliomalizika na sasa itashiriki Championship kwa msimu ujao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad