Manara Aibuka Kwa Mara Kwanza Baada ya Kufungiwa na Kusema Hayana Kwa Uchungu



Baada ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ kumfungia Msemaji wa Young Africans, Haji Sunday Ramadhan Manara miaka miwili na kumtoza Faini ya Shilingi Milioni 20, ametoa kauli yake ya kwanza.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, muda mchache baada ya hukumu, Manara aliandika kwa kifupi akimshukuru Mungu.

Manara ameandika: “Iwe ni jambo la kheri au shari, neno langu kuu ni kumshukuru Muumba wa Mbingu na Aridhi kwa neno moja kubwa na lenye maana pana sana Al-Hamdulilah.” ameandika Manara

Katika ujumbe huo Manara aliambatanisha na picha ambayo amevalia koti ka njano na jezi ya Young Africans akiwa amebeba Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Young Africans ilinyakua mataji mawili la Ligi Kuu Bara na Kombe la ASFC ikiifunga Coastal Union fainali ilipigwa Julai 2, Uwanja wa Amri Abeid Jijini Arusha.

Huko ndiko chanzo cha kesi hiyo kati ya Manara na Rais wa TFF, Wallace Karia ambapo leo Julai 21 amekutwa na hatia ya kutoa maneno yasiyofaa na kupewa adhabu ya kufungiwa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad