Maombi ya Zumaridi yakosa majibu mahakamani

 


Maombi ya mshtakiwa Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi ya kutokuwa na imani na hakimu anayeendesha kesi namba 10 ya kujeruhi askari na kumzuia afisa ustawi kutekeleza majukumu yake yameshindwa kupata majibu baada ya Hakimu huyo kudai alipata changamoto ya kiafya.


Mapema leo hii mfalme Zumaridi alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Monica Ndyekobora, ili kusubiri maamuzi ya maombi aliyotoa siku ya tarehe 11 ya mwezi huu ya kutokuwa na imani na Hakimu huyo,


Wakili wa serikali Emmanuel Luvinga ameiambia mahakama hiyo kuwa Zumaridi na wafuasi wake nane wapo tayari kwa ajili ya kupokea maamuzi ya mahakama ndipo Hakimu Monica Ndyekobora, akasema maamuzi hayo bado hayajafanyika kutokana na yeye kupata changamoto ya kiafya na kupanga tarehe nyingine ya kutoa maamuzi hayo ambayo ni tarehe 27 ya mwezi huu.


Aidha katika kesi nyingine namba 11 inayomkabili Zumaridi peke yake ya kuwatumikisha watoto wadogo wakili wa serikali Emmanuel Luvinga ameiambia mahakama hiyo kuwa upelelezi wake bado haujakamilika na mahakama hiyo ikapanga tarehe nyingine ya kesi hiyo kusomwa ambayo Agosti Mosi, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad