Cristiano Ronaldo ameomba kuondoka kwa mkopo kwenye klabu yake ya sasa ya Manchester United
SAKATA la mshambuliaji wa Manchester United ya nchini Uingereza Cristiano Ronaldo limechukua sura mpya mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika jana baina ya mchezaji huyo, wakala wake pamoja na Uongozi wa klabu hiyo akiwemo na Kocha Mkuu wa Timu hiyo Erik Ten Hag.
Ronaldo ambaye ni mshindi wa Ballon D’ Or mara tano pamoja na kuwa mfungaji bora wa muda wote kwenye mashindano ya Ligi Kuu ya Mabingwa Barani Ulaya ametoa masharti ya kuongezewa mkataba kasha kutolewa kwa mkopo kwa timu inayoshiriki ligi ya mabingwa.
Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba Wakala wa mchezaji huyo George Mendez ameiambia Manchester United kuwa inatakiwa kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja mchezaji huyo kasha imtoe kwa mkopo kwenye klabu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya halaf atarudi klabuni hapo kama klabu hiyo itafanikiwa kufuzu kushiriki ligi ya mabingwa msimu ujao.
Ronaldo alikuwa mfungaji Bora wa Manchester United msimu uliopita akiwa na jumla ya mabao 24 katika mashindano yote
Msimamo wa Manchester United umekuwa ni kwamba mchezaji huyo hauzwi ingawa inasubiriwa kuona kuwa kwa masharti hayo Manchester United itaamua nini.
Ronaldo ambaye alikuwa mfungaji bora wa klabu hiyo kwa kufunga jumla ya mabao 24 katika mashindano yote msimu uliopita, amebakisha kipindi cha mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa na Manchester United