Maskini...Mbwana Samatta Kupigwa Bei Fenerbahce Hayupo Katika Mipango ya Kocha




MIAMBA ya soka la Uturuki, Fenerbahce imemweka sokoni mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta baada ya kuonekana kutokuwa kwenye mipango ya Jorge Jesus.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Uturuki inaelezwa Jesus alipata wasaa wa kumtazama Samatta ambaye mkataba wake unamalizika Juni 30, 2024, kwenye maandalizi ya msimu ujao lakini ameonekana kutovutiwa na nahodha huyo wa Taifa Stars.

Awali kocha huyo mpya wa Fenerbahce aliagiza wachezaji waliotolewa kwa mkopo akiwemo Samatta ambaye aliichezea Royal Antwerp, kuwahi kuripoti kambini ili kuona kama kuna ambao viwango vyao vinaweza kumshawishi.

Kitendo cha Samatta kushindwa kumshawishi kocha huyo wa Kireno kwenye maandalizi ya msimu ujao, kimewafanya vigogo wa timu hiyo, kuamua kusikiliza ofa ya timu ambazo zipo tayari kupata huduma yake.


Chanzo kimoja ndani ya klabu hiyo, kimebainisha kuna ofa nzuri mbili ambazo zimewasilishwa kwa ajili ya Samatta zote ni kutoka Saudi Arabia. Hata hivyo, majina ya timu hayakuwekwa wazi. Changamoto inaelezwa ni utayari kwa mshambuliaji huyo kwenda kucheza soka Uarabuni.

Licha ya kutangaziwa mshahara mkubwa zipo taarifa Samatta anajiona bado ana uwezo wa kuendelea kucheza Ulaya na sio Asia ambako ushindani wake ni mdogo na wachezaji wengi huenda huko kumalizia soka lao.

Mbali na Samatta wachezaji wengine ambao wameonyeshwa mlango wa kutokea Fenerbahce ni pamoja na Caulker, Lemos, Meyer, Berisha, Gustavo na Novak.


Kama atapigwa bei dirisha hili la usajili, Samatta atakuwa amefuata nyayo za Ozan Tufan na Allahyar ambao walijiunga na Hull City kwa Euro 7.5 milion.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad