Mbunge wa Nzega Vijijini Hamisi Kigwangalla ambaye pia ni Mwanachama wa Club ya Simba amesema hana ugomvi na Mtu isipokua anachotaka kuona kikifanyika ni uendeshaji ulio wazi ndani ya Club ya Simba na kwamba anachofanya sasa ni kuitumia haki yake ya kikatiba ibara ya 100 na ibara ya 18.
Kigwangalla ameandika "Sina ugomvi na Mtu, ningekuwa na ugomvi mfano na Mooo ningemshambulia yeye ‘binafsi’ akini sijafanya hivyo, hata pale aliponidhalilisha sikumlipizia, ninachotaka ni mifumo ya uendeshaji iwe wazi bila janjajanja, natumia haki yangu ya kikatiba ibara ya 100 na ibara ya 18"
Vilevile Kigwangalla amesema amepigiwa simu na Mwenyekiti wa Simba SC. kupewa updates juu ya mambo mengi ya Club hiyo na nina mnukuu alichoandika "Mwenyekiti wa Bodi ya SimbaSCTanzania amenipigia kunipa updates juu ya mambo mengi ya klabu yetu, pamoja na kwamba kuna baadhi ya mambo sikuridhishwa na yalivyowekwa hususan yale ya kiuwekezaji....... ya usajili yako vizuri sana tu, walau ameonesha ujasiri, uwazi na weledi wake"