Mchezaji huyo ambaye aliwahi kupita katika klabu ya Simba, ameonesha kiwango cha hali ya juu msimu huu akiwa na klabu ya Coastal Union.
Mwishoni mwa wiki iliopita, mchezaji huyo akiitumikia Coastal Union, alifanikiwa kufunga mabao matatu pake yake kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Yanga huku ukimalizika kwa sare ya mabao 3-3 kabla ya Yanga kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya penalti.
Hata hivyo, Sopu kabla ya kujiunga na Azam FC alikuwa anahusishwa kutua Yanga SC au kurudi Simba, lakini Azam wameonesha ubabe wao.
Azam FC msimu ujao unadhani itakuwa ya aina gani?