Mchezaji Sopu Ang'ara, Stars Mwendo Mdundo CHAN



TIMU ya Taifa Stars imeendeleza ubabe mbele ya Somalia baada ya kuifunga mabao 2-1 katika mchezo wa pili wa marudiano uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo huo ni wa kufunzu fainali za Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) yatakayofanyika mwakani nchini Algeria.

Stars ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji, Abdul Suleiman 'Sopu' dakika ya 34 baada ya kupiga shuti kali lililomshinda kipa wa Somalia Abdirahman Mohamud.

Kipindi cha pili Somalia ilishambulia lango la Stars na dakika ya 48 ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Farhan Mohamed.


Stars chini ya kocha mkuu, Kim Poulsen alifanya mabadiliko kwa kumtoa George Mpole, Kibu Denis na Salum Abubakar huku nafasi zao zikichukuliwa na Anwar Jabir, Farid Mussa na Mudathir Yahya.

Mabadiliko hayo yalileta tija kwa Stars ambayo iliandika bao la pili kupitia kwa Dickson Job dakika ya 64 baada ya Sopu kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari.

Kwa matokeo haya yanaifanya Stars kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 3-1 baada ya mchezo wa kwanza uliofanyika Julai 23 kushinda 1-0.


Stars sasa itacheza na Uganda kwenye hatua ya mwisho ya mtoano ambapo mchezo wa kwanza utapigwa kati ya Agosti 26-28 huku marudiano yakifanyika kati ya Septemba 2-4.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad