Mchezaji wa Simba Peter Banda Kinda bora Afrika



NYOTA wa Simba, Peter Banda amechaguliwa na Shirikisho la Soka Afrika ngazi ya mashindano ya klabu kwa maana ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika kama kinda bora akiyefanya vizuri kwenye michuano hiyo msimu uliopita 2021/2022.

Banda mwenye umri wa miaka 21 ametajwa sambamba na makinda wengine watatu Mkongomani Guy Mbenza (22) anayecheza kwa mkopo Wydad Casablanca kwa mkopo akitokea Royal Antwerp ya Ubelgiji aliyokuwa akiichezea Mtanzania Mbwana Samatta msimu uliopita.

🇪🇬 Ahmed Abdelkader
🇨🇬 Guy Mbenza
🇲🇦 Mouad Fekkak
🇹🇿 Peter Banda

Upcoming young stars that excelled the 21/22 season!

Wengine ni Mmisri Ahmed AbdelKader (23) anayecheza Al Ahly Mmorocco, Mouad Fekkak anayekipiga RS Berkane ya nchini kwao huko.

Banda alisajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu uliomalizika akitokea Sheriff Tiraspol alikokuwa kwa mkopo akitokea Big Bullets ya nchini kwao Malawi ambayo ndio ilimuuza kwa Wekundu wa Msimbazi hao.

Huenda Banda msimu ujao akafanya makubwa zaidi katika michuano hiyo baada ya Simba kumaliza ligi katika nafasi ya pili na kujihakikishia kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo itaanzia hatua ya mwanzo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad