Mchungaji Afariki Akiongoza ibada ya Mazishi



Mchungaji wa Kanisa Katoliki kijiji cha Liputu, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Laurence Milanzi amefariki Dunia maeneo ya makaburini alipokuwa akishiriki mazishi ya mwanakijiji mwenzao aitwae Daudi Veno
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mchingaji huyo alianguka ghafla wakati akiwaasa watu kutosusia misiba kwa mtu asiyehudhuria Nyumba za Ibada

Kifo cha Mchungaji huyo kimetokea kwenye Kijiji hicho Julai 19 mwaka huu, saa 5:00 asubuhi kwenye eneo linalotumika mahususi kwa mazishi ya watu wanaofariki dunia.

Mwili wa Mchungaji huyo umehifadhiwa katika Hosptali ya Mission ya Ndanda, Wilaya ya Masasi ukisubiri taratibu za mazishi yanayotarajiwa kufanyika Kijiji hapo, baada ya kukamilika kwa taratibu zote.

Baadhi ya mashuhuda walioudhuria mazishi ya Daudi Veno, wameeleza kwamba, Mchungaji Milanzi amekutwa na umauti huo, alipokuwa anatoa sala na kuwasihi viongozi wenzake wa Dini kuacha tabia ya kutohudhuria mazishi kwa Binadamu mwenzao asiyeshiriki masuala ya Ibada.


Mchungaji Milanzi alisema kitendo cha kususa kumuombea marehemu kwa kuwa hakuwa anashiriki kwenye Nyumba za Ibada, Kanisani na misikitini ni kwenda kinyume na maagizo ya mwenyezi Mungu alivyoagiza mtu anapofariki ni muhimu akazikwa na sio kumuacha kwani uharibu hali ya hewa kutokana na harufu mbaya kutoka kwake.

“Baada ya kueleza hayo, tukamuona mwenzetu akidondoka chini kisha kupoteza fahamu” Walieleza Joseph Michael na Samwel Chindonga.

Aidha,mashuhuda hao wamesema kwamba baada ya Mchungaji huyo kudondoka chini walimchukuwa na kumkimbiza Hosptali ya Ndanda na kuelezwa na madaktari kuwa alishafariki


Mmoja wa madaktari wa Hosptali hiyo ya Ndanda ambaye hakupenda jina lake litajwe kwenye vyombo vya Habari (Dr Venance Chingwile) amethibitisha kupokelewa mwili wa Mchungaji Milanzi, na kuhifadhiwa chumba cha maiti (Mochwari) ukisubiri taratibu za mazishi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad