Mchungaji Awateka Nyara waumini ‘Awalamba Kisogo’ ni Kinyakuo

 


Jeshi la Polisi katika jimbo la Ondo lililopo nchini Nigeria, limefanya uokoaji wa watu 77 waliokuwa hawajulikani walipo mara baada ya kumalizika kwa ibada katika Kanisani la Whole Bible Believers Church, ambalo Mchungaji wake aliwateka nyara waumini wake akisema hiyo ni njia ya unyakuo.


Afisa Uhusiano wa Polisi wa jimbo hilo, SP Funmilayo Odunlami amesema waathiriwa hao walidanganywa na Mchungaji na Mchungaji Msaidizi Josiah Peter Asumosa, wa Kanisa hilo la mji huo kuwa siku za unyakuo zi karibu na hivyo watoe hofu.


Amesema baadhi ya watoto waliotekwa nyara na kuhifadhiwa katika shimo la kanisa katika hilo la Makao Makuu ya eneo la Serikali ya Mtaa wa Ondo Magharibi, waliokolewa na Polisi.


Police wa nchini Nigeria wakiwajibika katika moja ya matukio ya kiuhalifu.

RC aagizwa kuwashughulikiwa wafugaji wakorofi

“Wanahabari walikuwa wameripoti jinsi waathiriwa walivyokolewa siku ya ijumaa usiku katika eneo la Kanisa kwenye mhimili wa Valentino wa mji huo.


Odunlami alifichua kuwa miongoni mwa waathiriwa ni watoto 26, vijana 8 na waumini 43 wa kanisa hilo ambapo uokoaji ulifanywa kufuatia ripoti ya kijasusi iliyokusanywa na maafisa wa polisi katika Kitengo cha Fagun.


Asumosa ameongeza kuwa, Mchungaji huyo alikuwa amewatahadharisha waumini hao kwamba kutakuwa na unyakuo mwezi wa Aprili ambapo baadaye alisema kuwa umebadilishwa siku na hivyo utakuja Septemba, 2022.


Inasemekana kwamba kasisi huyo aliwaambia zaidi washiriki wake wapya wa Kanisa lake watii amri ya wazazi wao wa kiroho na si wazazi wao halisi.


Wakati huohuo, familia ya mmoja wa wahanga waliokuwa eneo la tukio wakati askari Polisi walipofika eneo hilo imesema binti yaoambaye ni mwanafunzi, aliacha shule kutokana na mafundisho ya ajabu ya Mchungaji huyo.


Walisema binti yao aliondoka nyumbani tangu Januari, 2022 na amekuwa akiishi Kanisani, huku akieleza kuwa uchunguzi umeanza na matokeo yake yatajulikana kwa umma, ingawa Odunlami alisema wachungaji wawili waliohusishwa na kitendo hicho wanashikiliwa na Polisi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad