Katika Jiji la Rio de Janeiro Nchini Brazil miaka 1980 na 1990 kumewahi kutokea mchezaji mmoja wa mpira wa miguu kwa jina Carlos Henrique Raposo lakini baadae aliamua mwenyewe kujibadilisha jina na kujiita ‘Kaiser’.
Kaiser alikuwa Mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa sana ndani ya Uwanja na kubahatika kusajiliwa zaidi ya Klabu 13 za Amerika ya Kusini na Nchini kwake Brazil lakini hakuwahi kucheza hata Mechi moja kwenye timu zote hizo, hapa ndipo tunaposema huyu ni mchezaji wa ‘Mchongo’.
Akiwa kwenye mazoezi Kaiser, ni tishio kweli kweli, kiasi kwamba mpaka kupelekea kupewa mikataba kirahisi na kuaminika na mabosi wa Klabu lakini kilichopelekea kutocheza hata Mchezo mmoja kwenye timu zote hizo alizowahi kusajiliwa ni kutokuwa tayari kucheza, akitumia mbinu za kudanya kuwa ana majeraha aliyopata mazoezini hasa mechi inapokaribia.
Sifa yake kubwa alikuwa akiingia mikataba mifupi mifupi na Klabu, akiwa mazoezini kiwango chake ni cha sayari nyingine, siku ya mechi anatangaza ni majeruhi, mkataba mpaka unakwisha hajacheza hata mechi moja na kuhamia timu nyingine eneo la mbali na timu yake anayoachana nayo.
Wakati mwingine hutumia CV za kuhama klabu nyingine kwa kigezo kuwa alikosa namba, huku akiwa na tabia ya kuwa karibu na waandishi wa habari, wachezaji na wamiliki wa klabu kote huko akitembeza uongo.
“Nilitaka kuwa miongoni mwa wachezaji wengine. Sikutaka kucheza. Ni shida ya kila mtu, walitaka niwe mwanasoka. Hata Yesu wapo ambao hawakupendezwa naye, kwa nini nifanye mimi ?,”- maneno ya Kaiser.
2015, Kampuni kutoka Uingereza ili nunua haki za ‘exclusive’ na kutengeneza ‘documentary’ iliyo wahusisha wachezaji wakubwa wa Brazili ambao walikuwa na Kaiser, kama Carlos Alberto, Zico, Junior, Bebeto, Renato Gaucho na wengine wakimzungumzia Carlos Henrique Raposo (Kaiser) Mshambuliaji wa kiwango cha Dunia na kusajiliwa zaidi ya Klabu 13 lakini hakuwahi kucheza hata mechi moja.
Bebeto, mshindi wa World Cup ya mwaka 1994, amesema “Alikuwa na maneno matamu, ukimuacha tu azungumze lazima uvutiwe naye, alikuwa mcheshi huwezi kumuepuka.”
Kwenye mazoezi ya kwanza tu, Kaiser tayari amesema ana majeraha ya misuli ambayo yangemfanya kuwa nje ya timu lakini muda wote akizunguka na kuleta utani, stori za kuchekesha mpaka mnasahau,” amesema Alexandre Torres mchezaji wa zamani wa Brazil. Carlos Alberto. “Atawapigia habari za kufurahisha, malengo ya wachezaji nadhani hiyo ndiyo sababu ya watu kumpenda mno.”
Katika siku hizo, kabla ya ‘internet’ hakuna mtu aliyekuwa na hekima zaidi. Ingawaje ingewezekana kumfatilia lakini jiji la Rio halikuwa na maeneo mengi zaidi.
Timu moja iliwahi kuchanganyikiwa na majeraha ya Kaiser ndipo ikamuita mchezaji huyo na Dokta wote kwa pamoja, lakini ghafla Kaiser akawa mkali kambwambia dokta na timu yake kuwa kuna magonjwa hata Uchawi hauwezi kutibu na kumtimua muuguzi huyo, lengo lake likiwa ni lile lile kukwepa kucheza.
Renato Gaúcho, Kocha na Winga wa zamani wa Brazilian ambaye amewahi kuwa kwenye kizazi cha Kaiser pamoja amemzungumzia mchezaji huyo kama “the greatest footballer never to have played football”
Hakika vituko vya Carlos Henrique Raposo ‘Kaiser’ ni vingi kamwe hatuwezi kuvimaliza.