Michael mwigizaji wa nchini Ghana anasema michepuko ya kike inapaswa kupongezwa kwa madai kwamba ndio inayosaidia ndoa ziendelee kudumu
Anadai michepuko inafanya kazi ya ziada kumfanyia mwanaume mambo kadhaa wa kadhaa ambayo hayapati kwa mke wake
Ameeleza kwamba wanawake wengi wakishaolewa tu wanajiachia sana na kusahau majukumu yao, pia amesema wake za watu kuna mambo wanasahau au kupuuza kumfanyia mwanaume wakidhani hayana umuhimu ila yanayo umuhimu, mfano kumsifia mume wake, kumfanyia vitu vya kufurahisha n.k
Amesema michepuko huwa inajiongeza sana na hivyo kuchochea ndoa ziendelee kuwepo mume akisharidhika kwa mchepuko anarudi kwa mke ambaye yupo yupo tu hivyo kuendelea kuitwa wanandoa hata kama ni wanandoa hewa