Morrison Atoa Ahadi Nzito Yanga “Nilisababisha Maumivu”




Kiungo wa kimataifa wa Ghana aliyejiunga na Yanga SC kama mchezaji huru akitokea Simba SC Benard Morrison ameandika ujumbe mzito kwa mashabiki wa Yanga ambao walihumia na kuondoka kwake na kujiunga na Simba SC sasa anasema amerudi nyumbani.

“Nilikuwa hapa nikaondoka sasa nimerudi tena naamini ujio huu wa pili utakuwa mkubwa kuliko ule wa mara ya kwanza nilipendwa na taifa hili la rangi ya njano na kijani na bado mnanipenda”

“Najua nilisababisha maumivu na aibu bado mmenikubali mtoto wenu nirudi nyumbani, sababu sote tunajua msemo wa nyumbani kutamu kijana wenu nimerudi na nitafanya niwezavyo kuwafanya muwe na furaha kila mahali na wakati wote”

“Tushirikiane kuiweka club hii kubwa kwenye jukwaa la kimataifa kama ilivyokuwa ikifanya hapo awali”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad