Msemaji Haji Manara Ashinda Kesi


Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa ya Mfanyabiashara Al Masoud kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyompa ushindi Msemaji wa Yanga, Haji Manara katika kesi ya madai kuhusu Perfume.

Rufaa hiyo namba 321 ya mwaka 2021 imetupiliwa mbali leo July 11, 2022 mbele ya Jaji Mango na kumpa ushindi Haji Manara ambapo katika rufaa hiyo Al Masoud aliwasilisha hoja kuu nne lakini Jaji Mango alisema hoja hizo hazina mashiko na anazitupilia mbali.

Katika shauri hilo @hajismanara aliwakilishwa na Wakili Claudio Msando.

Awali katika kesi hiyo ambayo ilifunguliwa Mahakama ya Kisutu, Abu Al Masoud alidai kuwa na mkataba na Haji Manara katika usambazaji wa Perfurme iitwayo De La Boss ambapo Manara na wenzake wawili Beatrice Ndungu na Palm General Supply walishtakiwa kwa kupokea perfume hizo bila kuzilipia hivyo Mfanyabiashara huyo alitaka fidia ya Tsh milioni 83.3.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad