Msuva apanga matumizi ya Sh1.6 bilioni




MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Saimon Msuva amesema baada ya Mungu kumtendea na kupata haki yake, atatoa fungu la 10 kanisani.
Juzi shirikisho la soka Duniani FIFA lilitoa hukumu ya malalamiko ya Msuva dhidi ya ilivyokuwa timu yake ya Wydad Casablanca ya Nchini Morocco.

FIFA imeipa siku 15 Wydad kumlipa Dola za kimarekani 700,000 sawa na Sh1.6 bilioni zikitakiwa kulipwa kwa staa hiyo ikiwa ni sehemu ya mishahara na hela ya usajili.

"Nitatoa fungu la 10 kanisani kumshukuru Mungu kwa kupokea maombi yangu, ni karibu mwaka nipo tu lakini niliamini kwa uwezo wake Mungu haki yangu nitaipata," amesema Msuva.

Aidha Msuva amesema hakutaka kusikiliza maneno ya watu mitandaoni waliomuona Kama amepotea kukaa bila timu.
"Mimi najua na naelewa sikutaka kukurupuka zipo timu nyingi zilinitaka lakini sikuwa na haja ya papara nilijua siku ipo na itafika, "anasema Msuva.


 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad