Msuva: Rais wa Timu Alikuwa Hapokei Simu Zangu, Nilimuombea Afe





Simon Msuva amesema amepata uzoefu wa kutosha kutokana na sakata lake dhidi ya klabu ya Wydad Casablanca
MSHAMBULIAJI wa Timu ya Taifa ya Tanzania Simon Msuva ambaye alikuwa akikipiga katika Klabu ya Raja Casablanca amefunguka magumu aliyoyapitia wakati akihudumu katika klabu hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari Msuva amesema ilifikia wakati akaamua kumpigia hadi simu Rais wa Wydad Casablanca ili apate nafasi ya kuongea naye kuhusu sakata lake la kutolipwa haki zake ikiwemo pesa za malimbikizo ya mishahara pamoja na pesa ya usajili.


Msuva amesema Rais wa Wydad alikuwa hapokei simu zake
Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida Msuva amebainisha kuwa Rais huyo alikuwa hapokei simu yake na pia anatoa maelekezo kwa walinzi kutomfungulia geti mchezaji huyo.

“Kweli mi nimeishi nao wale watu ilifikia kipindi mpaka nikampigia simu Rais wa Timu nionane naye alikuwa hapokei simu na sometime ananambia njoo nyumbani kwangu na nafika hadi nyumbani kwake na sometime yuko ndani lakini getini pale anawaambia walainzi, waseme hayupo nyumbani ametoka.”



Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Simon Msuva
Msuva ameendelea kwa kusema kuwa nchi za kiarabu zina usumbufu nay eye tayari amejifunza kutokana na tukio hilo na hata akiondoka kwenda sehemu nyingine yoyote basi atakuwa anajua pa kuanzia na pa kuishia huku akisistiza kuwa kuna muda ulifika hadi akawa anamuombea Rais yule afariki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad