Tumebarikiwa wasanii wengi, lakini @diamondplatnumz anabaki kuwa msanii bora kuwahi kutokea kwa miaka 13, katika muziki wa bongo fleva akicheza miguu yote miwili inayomfanya abaki kuwa juu siku zote.
Diamond ni mwimbaji na mtunzi mzuri wa muziki mwenye uwezo wa kiushindani na wasanii wa mataifa ya nje, msanii ambaye amechukua tuzo nyingi na nimoja wa wasanii wanaolipwa fedha nyingi katika kutumbuiza jukwaani.
Amekuza na kuinua vipaji vipya vya wasanii wachanga na hata kuwainua wale aliyowakuta katika game kwa namna moja ama nyingine, kama sifa tumpe kama anavyo stahili kupewa.
Mafanikio kimuziki na nje ya muziki basi jamaa kayapata na anaendelea kukaza maana game inawapinzani sana, wapo wasanii ambao wanafanya vizuri sana Harmonize, Marioo hawa ni miongoni mwa watanzania katika kupeperusha bendera ya nchi katika mataifa ya nje.
Sanaa ya bongo fleva inakuwa kwa kasi sana ukilinganisha na miaka ya nyuma utaona tofauti, wapo vijana wa kuwaangalia kwa jicho la tatu sio swala lakuwapa muda bali kuwasapoti ili game izidi kukua zaidi ya hapa ilipo sasa.
✍️ Na @mtumakiniart