Museveni na Kauli Tata Kwa Waganda

 


Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amewahimiza raia wa taifa lake kuhamia kwenye magari yanayotumia umeme kwa kuwa mafuta yanazidi kuwa ghali.


Kauli hiyo imekuja kutokana na hali mbaya ya uchumi wa dunia ambayo imeshuhudia bei za bidhaa mbalimbali zikipanda kwa viwango ambavyo wengi hawawezi kumudu.


Kauli yake inajiri wakati ambapo bei ya mafuta imepanda kwa kiasi kikubwa ambapo kwa sasa lita moja ya petrol nchini humo inauzwa takriban shilingi 7,000 pesa za Uganda sawa na shillingi 4,273.87 ya kitanzania huku chini ya asimilia mbili pekee ya milioni 44 ya raia wa Uganda ikiwa na uwezo wa kumiliki motokaa.


“Hili ndilo jibu. Njia sahihi ni kuanza kuondokea petrol na kukumbatia magari yanayotumia umeme na tayari tumeanza,” Museveni alisema.


Museveni aliongeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa bei ya mafuta kubaki kuwa juu kwa muda mrefu hata taifa hilo linapozidi kutafuta mbinu za kupata mafuta yake.


Alielelezea imani kwa hali ya taifa hilo kufufua reli zake ili raia wa taifa hilo wanapochoshwa na bei ya juu ya mafuta watatumia treni.


Mwezi uliopita Rais huyo aliwataka waganda wale mihogo kama bei ya mkate imewashinda na kuacha kujihangaisha.


Museveni alidai kuwa mfumko wa bei ya bidhaa nchini humo umesababishwa na ugonjwa wa Korona na vita kati ya Urusi na Ukraine ambavyo vimetatiza uchukuzi wa mizigo na kusababisha uhaba.


“Kama hakuna mkate basi kula mhogo. Waafrika hujikanganya sana. Unalalamika kuwa hakuna mkate au ngano, tafadhali kula mhogo. Mimi mwenyewe sili mkate,” Museveni alisema katika sherehe za Leba Dei jijini Kampala.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad