Mahakama nchini Misri imetoa hukumu ya kunyongwa kwa Mtuhumiwa Mohamed Adel (21), huku akionyeshwa kwenye Televisheni nchini humo baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya mauaji iliyokuwa ikimkabili.
Mohamed Adel alipatikana na hatia ya kumuua Mwanafunzi mwenzake wa kike Nayera Ashraf nje ya Chuo Kikuu cha Mansoura kaskazini mwa Misri mwezi uliopita baada ya binti huyo kumkatalia ombi lake alipomtongoza.
Mahakama imeliandikia barua bunge la Misri kuruhusu kunyongwa kwa Mohamed kurushwe moja kwa moja kupitia matangazo ya televisheni nchini Misri ili kuzuia matukio ya kihalifu kama hayo kutojirudia tena.
Tukio la mauaji ya mwanafunzi Nayera lilisambaa kupitia video katika mitandao ya kijamii na kuzua hasira nchini humo huku mamlaka zikilaumiwa kwa kutochukua hatua kali dhidi ya vitendo vya kiunyanyasaji dhidi ya wanawake.
Shirika la Amnesty International lilitoa ripoti mwaka jana kwamba polisi nchini Misri kutochunguza vya kutosha unyanyasaji wa kingono na kijinsia kwa wanawake na mahakama hazitoi adhabu za kutosha.