Mwanajeshi mstaafu aua wakigombea mpaka




MSTAAFU wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jonas Ziganyige (71), anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kumpiga risasi na kumuua mfanyabiashara, Patient Romward (48).

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, Jumanne Muliro, amesema hayo leo na kuongeza kuwa baada ya tukio mtuhumiwa alikimbia, lakini alikamatwa eneo la Kibaha Maili Moja.

 Amesema  mstaafu huyo mkazi wa Mbezi Juu, alifanya mauaji hayo, Julai 9,2022  saa 4 asubuhi,  baada ya Patient ambaye ni mkazi wa Wazo Mivumoni, Kinondoni kufika eneo hilo kwa lengo la kukagua mipaka ya kiwanja chake.

Kamanda amesema marehemu alifika eneo hilo akiwa na mwenzie  Recy Renso (52)  na mtuhumiwa  alitoka ndani huku akionesha kukasirishwa na hatua ya watu hao, akachukua bunduki na kumpiga risasi Romward.


 
Amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia, lakini upelelezi umefanywa na Julai  10,2022 alikamatwa eneo la Kibaha Maili Moja akiwa amejificha.

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, pia limeipata silaha aliyotumia mtuhumiwa, ambayo ni aina ya Mark IV, ikiwa na risasi nne.

Pia katika tukio lingine  jeshi hilo limewakamata watuhumiwa nane sugu wa  matukio ya uvunjaji nyumba na kuiba  vifaa vya magari, akiwemo Jumanne Omary (28), mkazi wa Mikwambe na wenzake  saba wamekamatwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad