Mwimbaji Peter Okoye wa Square Ajitoa Katika Kampuni

 


Mwimbaji Peter Okoye ambaye ni mmoja wa kaka wawili wanaounda kundi la muziki la P Square amesema kwamba amejiondoa kama mtangazaji wa kampuni yake ya bahati nasibu iitwayo ‘Zoom Lifestyle’ au ‘Zoom Up Your Life’.


Awali alikuwa ametoa ujumbe wa kujiuzulu bila maelezo ambao ulichukuliwa ndivyo sivyo na mashabiki wake. Wengi walidhania kwamba anajiondoa kwenye kundi la P Square ambalo wamefufua miezi kadhaa iliyopita.


Mwimbaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema kwamba hatua yake imechochewa na matapeli ambao wamekuwa wakichukua video zake akitangaza washindi kwenye Instagram na kuzitumia kuibia watu wasio na habari mitandaoni.


Fahanu, kila Jumamosi, Peter alikuwa akifanya shindano hilo la bahati nasibu na kutangaza washindi mubashara kupitia Instagram yake ambapo huwapigia simu moja kwa moja na kuwatumia fedha. Anasema sasa hilo halitafanyika lakini mchezo huo utaendelea.


Alisema tiketi zote za kujiunga na mchezo zitaendelea kupatikana kwenye tovuti yao ya zoomlifestyle na wala sio kwa kutuma pesa kwenye akaunti fulani. Alifafanua kwamba, hawatumii mtandao wa Whatsapp

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad