Arusha. ZIKIWA zimesalia masaa matano kupigwa kwa mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mashabiki wa timu hizo wamejitokeza kwa wingi kuzipa sapoti timu zao.
Mchezo huo utaanza majira ya saa 9:00 alasiri ambapo Mwanaspoti limeshuudia umati mkubwa wa mashabiki wakijitokeza kwa wingi asubuhi kukata tiketi hili kuweza kushuudia mtanange huo.
Mbali na kiingilio cha chini kuwa sh 10,000 kwa mzunguko mashabiki hao kwao imeonekana hakuna shida kila mmoja amehamasika kutaka kuona timu yake inabeba ubingwa au mpinzani anabeba.
Kenneth Makotha ni shabiki wa Yanga kutoka Babati mkoani Manyara anasema matumaini yake ni makubwa sana kuelekea katika mchezo kwani kutokana na kikosi chake kilivyo lazima watabeba ubingwa wa pili mfululizo.
Anasema wala haiofii Coastal kwani ina wachezaji wa kawaida sana ukilinganisha na ubora wa Yanga kwa sasa kilivyo hivyo wao wamekuja kuwapa kikombe kingine.
"Mayele atatema wao wanasema wamemfunga najua kuna vingi vya kufunga ila siyo mwamba lazima tuteteme". amesema Makotha.
Kwa upande wake shabiki wa Coastal Union FC, Hussein Bakar anasema wametoka Tanga kuja kuchukua ubingwa na kupata tiketi ya kushiriki kimataifa msimu ujao hivyo ni lazima washinde.
Amesema Yanga waje wakiwa wamejipanga kabisa kwani wana hasira nao kweli kweli baada ya kutangaza ubingwa wa ligi kupitia wao.