Polisi Yapunguza Utitiri wa Trafiki Barabarani..Ushauri wa CCM Wafanya Kazi



JESHI la Polisi limesema limefanyia kazi ushauri uliotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana kuanzia leo Julai 29,2022 wa kupunguza trafiki barabarani ambao husababisha kero kwa wananchi.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime, inasema Jeshi la Polisi limeanza kuweka mikakati mizuri ya utekelezaji ambao pia umepokelewa kwa maoni mengi kutoka Kwa wananchi.

“Taasisi yeyote hasa inayohudumia jamii moja kwa moja kama Jeshi la Polisi, ili utendaji wake uweze kuboreshwa kila mara na uendane na matarajio ya wananchi na wadau wengine ni lazima kupokea ushauri, maoni na malalamiko na kuyafanyia kazi kwa wakati ili kuboresha utendaji wake na kuwaondolea kero wananchi,” amesema.

Adha, amesema Jeshi la Polisi lipo wazi kupokea maoni na ushauri kutoka kwa mtu yeyote mwenye lengo la kuboresha kitengo chochote au utendaji wa Jeshi la Polisi kwa ujumla ili wananchi wapate huduma bora pamoja na kupunguza malalamiko kama sio kuondoa kabisa


Kauli hiyo ya Jeshi la Polisi imekuja ikiwa ni saa chache baada ya Kinana kumshauri IGP Wambura kupunguza idadi ya matrafiki nchini.

Kinana alitoa ushauri huo mkoani Mbeya baada ya kupokea malalamiko ya wananchi yaliyoibuka katika kikao cha ndani cha wanachama wa CCM Mkoa wa Songwe ambao walitoa malalamiko mbele ya Kinana akidai wamechoka kusimamishwa mara kwa mara na trafiki na kila wanaposimama wanatoa sh. 2,000 kwa kila kituo.

“Lakini namuomba na kumshauri IGP atazame wingi wa trafiki mijini, kila baada ya muda mfupi unasimamishwa na trafiki, wenye magari hawaendeshi kwa raha, hivyo nimsihi IGP afanye tathimini kuhusu uwepo wa trafiki wengi kwenye miji yetu, wamekuwa wengi sana kila ukitembea kidogo unasimamishwa, kilomita moja unakuta trafiki.


“Namuomba IGP afanye tathimini watu wapumue, watu biashara zao zinaharibika kwa sababu ya kuambiwa paki pembeni, tunaheshimu umuhimu wa usalama nchini, lakini tunakerwa na kuambiwa paki gari pembeni. Namuomba IGP, naheshimu na natambua uwezo wake mkubwa, lakini afanye tathimini je, kuna umuhimu wa kuwa na idadi kubwa ya trafiki barabarani?´alihoji Kinana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad