Qnet Yawafukuzisha Kazi Walimu Wanane



TUME ya Utumishi wa Walimu wilayani Geita imewafukuza kazi walimu wanane kwa utoro kazini ambapo baada ya uchunguzi wamebainika walikuwa wanajishughulisha na biashara za Qnet badala ya kutumikia ajira zao.

Walimu hao ambao sita ni wa shule za msingi na wawili wa shule za sekondari, wanadaiwa kujishughulisha na biashara za Qnet badala ya kumtumikia mwajiri hadi kupelekea wengine kuathiriwa na biashara hizo baadaye kujikuta wanadaiwa na wafanyakazi wenzao waliowaingiza kwenye biashara hiyo.

Katibu Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu wilayani humo, Sitta Mussanga, amethibitisha kufukuzwa kwa walimu hao na kabla ya kufukuzwa tume iliunda kamati ya uchunguzi na kujiridhisha kuwa ni watoro kazini.

“Walimu waliofukuzwa kwa sababu utoro wao umesababishwa na Qnet wako wanane ambao walishatakiwa na waajiri wao kwa nyakati tofauti wapo wa Halmashauri ya mji na wengine Halmashauri ya Wilaya waliacha kazi wakaenda Qnet ambako wanaamini kuna maslahi mazuri kuliko huku kwenye ualimu," amesema Mussanga.

Amesema licha ya kuacha pengo kwenye shule walizokuwa wakifundisha kwa kusababisha uhaba wa walimu pia walikokwenda walichotarajia hawakukipata na baadhi wamepata msongo kutokana na kukabiliwa na madeni.


Akitaja shule zilizoathiriwa kwa walimu wao kufukuzwa, Mussanga alizitaja kuwa ni Kivukoni sekondari walimu wawili, shule ya msingi Nyantorotoro(2), Kivukoni ,Lubanda, Mtakuja na mkoani ambazo zote zimepoteza mwalimu mmoja mmoja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad