R. Kelly Aondolewa Ulinzi Mkali Gerezani..


Nguli wa muziki miondoko ya R&B, mwimbaji Robert Sylvester Kelly maarufu R. Kelly, ameondolewa ulinzi mkali aliokuwa amewekewa ili asijitoe uhai, baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani.


Kumekuwa na tetesi kuwa staa huyo wa Marekani, angejitoa uhai kutokana na msongo wa mawazo uliofuatia hukumu hiyo. Wasimamizi wa mashtaka walipendekeza msanii huyo aliye na umri wa miaka 55, awekewe ulinzi mkali maarufu kama "Suicide watch".


Waendesha mashtaka hapo awali walisema Kelly alihitajika kuwekwa kwenye uangalizi huu maalum kwa sababu ya usalama wake lakini mawakili wake walifungua kesi wiki iliyopita wakidai aliwekwa kwenye lindo hilo maalum kama adhabu na sio kusaidiwa.


Fahamu, "Suicide watch" hupewa mfungwa au mgonjwa ambaye yupo katika hatari ya kujiua.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad