Rais Paul Kagame Atangaza Kugombea Urais kwa Awamu ya Nne 2024 Nchini Rwanda

 


Rais Paul Kagame, mtawala mkuu wa Rwanda tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari mwaka 1994, amedokeza kuwa atagombea tena urais katika uchaguzi ujao wa 2024.

Alipoulizwa kama atagombea tena urais, Kagame alisema: “Nafikiria kugombea kwa miaka 20 zaidi. Sina tatizo na hilo,” alisema Rais Kagame

“Uchaguzi unahusu watu kuchagua,” aliongeza.

Kagame alibadilisha katiba mwaka 2015 na kumruhusu kubakia madarakani hadi 2034.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 64 alifagia uchaguzi wa urais wa 2017 kwa kupata asilimia 99 ya kura.

Alikuwa na umri wa miaka 36 tu wakati chama chake cha Patriotic Front kilipowafukuza Wahutu wenye msimamo mkali waliolaumiwa kwa mauaji ya halaiki ambapo takriban watu 800,000 hasa Watutsi waliuawa kati ya Aprili na Julai 1994.

Kagame alitetea vikali rekodi ya Rwanda kuhusu haki za binadamu na uhuru wa kisiasa katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola mjini Kigali mwishoni mwa Juni.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad