Rais Samia: Tutanunua vifaa vya treni vipya, mtumba



RAIS Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imetoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya treni ya kisasa, huku akisema miongoni mwa vifaa hivyo vitakuwa vilivyotumika. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, tarehe 4 Julai 2022, akishuhudia hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha nne kutoka Tabora hadi Isaka.

Rais Samia amesema, miongoni mwa vifaa vipya ambavyo Serikali imeweka oda kiwandani kwa ajili ya kutengenezwa, ni seti za treni za kisasa 10, vichwa vya treni vipya 17 na mabehewa ya abiria.

“Matarajio yangu kuanzia katikati ya 2023, baadhi ya hivi vitu kama sio mwishoni mwa mwaka huu, vingi tumekuwa tumevipokea na vingine tutakuwa tumevipokea 2023. Kwa nini? Kwa sababu vingi vitu tumeagiza,” amesema Rais Samia na kuongeza:


 
Rais Samia amesema “vipo vya kutengeneza, tutanunua vya kuanzia vilivyotumika lakini vyenye hali nzuri. Tutatengeneza ili reli ifanye kazi lakini tutakavyoviagiza tutavipokea  2023 na vitafanya kazi kwa muda mrefu zaidi.”

Aidha, Rais Samia ameliagiza  Shirika la Reli Tanzania (TRC), kuweka mipango ya biashara ili fedha zipatikane kwa ajili ya kulipa mkopo uliochukuliwa kwa ajili ya kuijenga. Reli hiyo inajengwa kwa gharama ya Sh. 16 trilioni.

“Tuhakikishe tunakuwa na mipango mizuri ya biashara hii ya usafirishaji. Tumeona vichwa vinapita na matumaini yetu kuanzia pengine mwakani katikati, Juni au Julai tutaanza kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodom, tuanze kuweka mipango ya kibiashara ya reli ili fedha iweze kurudi na kurudi kwa haraka ili  tuweze kulipa mkopo kwa haraka,” amesema Rais Samia.


Rais Samia amesema, ujenzi wa reli hiyo utasaidia kuunganisha mikoa tisa, ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Singida, Tabora na Simiyu, pamoja na nchi jirani za Uganda, Burundi, Rwanda na Sudani Kusini.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad