Rais wa Sri Lanka na Waziri Mkuu Wajiuzulu Kufuatia Maandamano Makubwa Kupinga Ugumu wa Maisha

 


Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa ambaye amekubali kujiuzulu wadhifa wake kufuatia maandamano makubwa yaliouzuka nchini humo.

SPIKA wa Bunge la Sri Lanka Mahinda Yapa Abeywardena ametangaza kuwa Rais wa nchi hiyo Gotabaya Rajapaksa amekubali kujiuzulu wadhifa wake kufuatia maandamano ya vurugu, Rajapaksa atajiuzulu 13 Julai 2022.

Hatua hiyo imekuja baada ya waandamanaji kumshinikiza Rais na Waziri Mkuu kujiuzulu, waandamanaji hao walivamia makazi ya Rais na kuchoma moto makazi ya kibinafsi ya Waziri Mkuu jijini Colombo, Waziri Mkuu Wickremesinghe pia amekubali kujiuzulu.

Spika wa bunge alisema Rais ameamua kujiuzulu “ili kuhakikisha makabidhiano ya amani ya mamlaka” na kutoa wito kwa umma “kuheshimu sheria” Tangazo hilo liliibua furaha na kupigwa kwa mafataki ya sherehe katika jiji hilo.

Maandamano nchini humo yamechochewa na mzozo wa kiuchumi ambao haujawahi kutokea na kusababisha uhaba wa mafuta, gesi, dawa na vyakula ambavyo Serikali imeshindwa kununua kutokana na ukosefu wa fedha.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad