RAIS wa Ukraine Volodymir Zelenskiy amewafuta kazi mkuu wa huduma za ujasusi na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali huyo amesema watu wapatao sitini wanaotumikia taasisi zilizoongozwa na maafisa hao waliotimuliwa, wanafanya kazi dhidi ya Ukraine katika maeneo yanayoshikiliwa na Urusi.
Zelenskiy amesema kesi 651 za jinai zimefunguliwa kuhusu makosa ya uhaini wa kiwango cha juu, zikiwahusisha wafanyakazi katika ofisi ya mwendesha mashtaka, vitengo vya kuchunguza kesi na taasisi nyingine za kisheria.
Kiongozi huyo wa Ukraine amesema visa hivyo vinaibua maswali magumu juu ya maafisa hao waliofukuzwa, na amesisitiza kuwa maswali hayo yatapata majibu sahihi.
Wakati huo huo jeshi la Urusi lilitangaza hapo jana kuwa limeziharibu silaha ambazo nchi za magharibi zimeipatia Ukraine, ukiwemo mfumo wa makombora wa Himars uliotolewa na Marekani hakuna upande huru uliothibitisha ukweli wa madai hayo ya Urusi.