Rayvanny Aaga Rasmi WCB, Amshukuru Diamond

 


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa lebo ya Next Level Rayamond Shabani alimaarufu Rayvanny ameaga rasmi katika label ya WCB Wasafi chini ya Diamond Platnumz.


Akiongea katika video ya dakika mbili aliyoitengeneza ameonyesha baadhi ya mambo aliyopitia na kufanikiwa akiwa chini ya WCB kwa takribani miaka 6 aliyoitumika pale.


Chini ya video hiyo Diamond amecomment na kuandika NEXT LEVEL PRESIDENT akionyesha kumpa baraka zote Rayvanny.


Rayvanny ameongea mengi sana ikiwa kwenda kuanzisha familia nyingine akimaanisha Next level na kusaidia wasanii wengine kama yeye alivyosaidiwa.


Unahisi ni wakati mzuri kwa Rayvanny kujiondoa WCB na kujisimamia mwenyewe?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad