Senzo "Nilimhofia Sana Benard Morrison Ila Nafurahi Hakuwa Kutufunga Yanga"



MTENDAJI Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amejikuta akicheka tu baada ya ndoto zake kutimia kufanya kazi na mshambuliaji Bernard Morrison.

Akizungumza na Mwanaspoti, Senzo alisema kama kuna ndoto tatu zimetimia kwake wakati akiwa Yanga ni kufanya kazi na Morrison ambaye alipishana naye wakati akija Yanga.

Itakumbukwa wakati Morrison anakwenda Simba hakufanikiwa kufanya kazi na Senzo ambaye naye alikuwa anaondoka akija Yanga kimyakimya katika uhamisho ambao uliweka historia.

Jana Senzo alifichua kwamba wakati anatoka Simba aliumizwa na hatua ya kupishana na raia huyo wa Ghana ambaye alihama kwa kishindo.


“Nilifanyia kazi kwa kiasi uhamisho wa Morrison akija Simba lakini wakati nikiwa Simba nilikuwa namuogopa sana alikuwa hatari sana siku ambayo aliifunga Simba niliumia sana na nikawaambia huyu jamaa watani wetu wamepata mtu hatari,”alisema Senzo.

“Nafurahi alipokwenda Simba hakufanikiwa kutufunga ningeumia zaidi ingekuwa kama ametonesha kidonda changu na sasa nilihakikisha anarudi hapa Yanga.

Senzo alisema Morrison ni mshambuliaji mzuri ambaye licha ya rekodi ya matukio yake amewataka Wanayanga kumpokea vizuri na kusahau ya nyuma.


“Mashabiki nawaomba mimi Senzo wasahau wampokee Morrison, watafurahia kazi yake huyu ni mchezaji.”


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad