Shaffih Dauda Aingilia Sakata la Haji Manara na Rais wa TFF "Manara Aombe Msamaha Hadharani"


Kwangu football ni zaidi ya mchezo, kwangu football ni familia na ni maisha yetu ya kila siku, yanayotukutanisha na kutupa faida, nautazama hivyo mpira

Nautazama mpira kama sehemu ya upendo, amani na mshikamano sehemu ambayo ni kiwanda cha ajira, ambapo watu wanalisha familia na maisha kusonga

Nimeiona clip ya Haji, akiwa kwenye majibizano na Rais wa TFF ambaye anaongoza chombo chenye mamlaka ya mpira wa nchi, Haji akiwemo ndani ya chombo hicho, nimeitazama vyema sana

Nakubaliana na nyote kuwa ni kweli Haji amekosea sana tena amekosea pakubwa kuikosoea mamlaka tena hadharani, ni kosa kubwa ambalo amelifanya kwa heshima ya mpira wa miguu

Lakini mimi namtazama Haji kwa jicho la binadamu, jicho la kukosea na kupatia, jicho la kutenda kosa na kujuta, namtazama kwenye jicho hilo, naitazama kama ajali kazini na kila Binadamu ana mapungufu

Mpaka sasa nilitarajia Haji awe ameomba radhi tena hadharani hata kama ameomba personally kama amefanya hivyo, hapo atakuwa ameupa heshima mpira wa miguu na heshima yake binafsi

Pamoja na kwamba amepelekwa kwenye kamati ya maadili ila binafsi yangu namuombea msamaha, msamaha wa kuwa pamoja ya kuwa ana makosa yake lakini bado ni binadamu

Bado mpira wetu unamuhitaji na ametoa mchango wake mkubwa, huwa sina raha kuona familia ya mpira ikiwa kwenye dhoruba, huwa sina amani kama familia ya mpira haipo na amani

Nakuombea hili lipite salama kwa heshima na kwa kadri kamati itakavyoona, mpira wa miguu haupaswi kupoteza Wanafamilia, tuendele kushikana pamoja tufike nchi ya ahadi, KIRI MAKOSA AND LETS MOVE ON

MUNGU ATUBARIKI SOTE

DIGALA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad