Ameandika haya Mchambuzi Mkubwa wa Michezo Tanzania Shaffih Dauda:
One of our own, ndio lugha sahihi zaidi kuweza kuitumia ndio mtoto wa Tanzania ambaye anasaka rizk yake kupitia mpira wa miguu, amebeba kiatu akitokea Geita Gold
One of our own, ndio neno sahihi kulitumia hapa! Ndio safari hii sio Simba, sio Yanga wala sio Azam ni kanda ya ziwa imetuletea Mfungaji bora akiwa na mabao 17, i like it
One of our won, a boy from the streets of Mbeya! Amekata kamba za kila aina kutoka kwenye zile zinazotambulika timu ndogo, kutoka kwenye timu ambazo wachezaji wake wengi ni wazawa
One of our own, ni mstari sahihi kuutumia! Ndio John Bocco amewahi kufanya, lakini hata yeye atakubaliana na Waandishi kuwa sio rahisi kufanya hivyo kwenye timu nje na tatu, lakini George amefanya
One of our own, ndio ni wetu! Ijapo watu watasema mbona Aiyee alifanya, mbona Mohamed Rashid alifanya! Lakini msisahau IDEAS ARE PRIMARY, AND MATTER IS DERIVATIVE OF IDEAS, wazo limekuja sasa ni lazima litekelezwe sasa, kwakuwa nyakati zinabadilika
Mdogo wangu @alikamwe na Waandishi wa michezo walikuja na wazo la kumpa Million moja kijana, ni sahihi sana! Hii itawaamsha watoto kutoka Iwambi, Mbeya au Rorya kule Mara, Chitohori kule Mtwara au Matombo, Morogoro kuwa hata ninyi mnaweza
One of our own, watu tu hawajiulizi iliwezekana vipi Raheem Sterling kununuliwa bei ghali pale Manchester City kuliko Kun Aguero, hawajiulizi kwanini Ahly ni ngumu kutoboa mgeni, simply ni kuwa their own need to be their priority
Nawapongeza wafungaji 10 bora wote, nawapongeza pasi na ubaguzi wowote ila @officiall_georgempole defied the odds just from the pitch of Nyankumbu
Nampa MILLION MOJA yake kama DIGALA na naamini Waandishi na Wadau watampatia MILLION MOJA yake nyingine
#TheFuture" Dauda