Sheria Ngowi Mbunifu wa Jezi ya Yanga....


Unapolitaja jina la Sheria Ngowi unamgusa moja ya wabunifu wakubwa Afrika anayewavalisha Viongozi wakubwa wa mataifa mbalimbali ndani na nje ya Afrika.


Pia ndio mbunifu namba moja Afrika kwa mavazi ya nguo za kiume akitunukiwa tuzo hizo mara tatu mfululizo haina ubishi kwa sababu anastahili. Sheria Ngowi ambaye ndiye aliyebuni jezi za Yanga za msimu uliopita wa 2021/22, ndiye mbunifu wa jezi mpya za mabingwa hao nchini kwa msimu ujao.


Sasa kupitia ukurasa wake wa Instagram Sheria Ngowi  amebainisha kuwa siku ya uzinduzi wa Jezi za Yanga kwa msimu mpya wa 2022/23 itatangazwa hivi Karibuni.


Sheria Ngowi anazidi kutuonesha watanzania kuwa kuna wabunifu wenye uwezo mkubwa sana ndani ya Tanzania na wanaoweza kufanya mambo makubwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad