Saa chache baada ya kumsikiliza Haji Manara akieleza kwa kina upande wake juu ya adhabu aliyopewa na Shirikisho la mpira wa miguu Tanazania (TFF), hatimaye shirikilo hilo limetoa taarifa mpya ikisikitishwa na madai yake.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amesikitishwa na madai ya Haji Manara kuwa alimuomba msamaha kwa maelezo kuwa Rais wa TFF, Wallace Karia alifanya makosa.
"Maneno hayo si ya kweli na Sekretarieti ya TFF haina nafasi ya kuendelea kuzungumzia jambo ambalo tayari limetolewa uamuzi na chombo huru cha TFF" - Kidao.
Julai 21 mwaka huu Kamati ya Maadili ya TFF ilimfungia Manara kujihusisha na mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili, na kumpiga faini ya Sh20 milioni kwa kosa la kumtishia na kumdhalilisha Rais wa TFF.