Simba wanne wahamishiwa Hifadhi ya Burigi-Chato



SHAMBA la Manyara Ranch lililoko mkoani Arusha limehamisha simba wake wanne na kuwapeleka katika Hifadhi ya Burigi iliyoko Chato kutokana na kuua watu katika eneo hilo.

Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa migogoro baina ya wanyamapori na wananchi.

Vilevile shamba hilo limeuza ng’ombe wake kwa wananchi katika mnada maalumu kutokana na hali mbaya ya hewa na kukosa chakula kwa ukame.

Meneja wa Ranchi hiyo, Fidelis OleKashe alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) waliotaka kujua hali halisi ya shamba hilo katika usimamizi na uhifadhi wa wanyamapori.


 
Waandishi hao wanatekeleza mradi unaofadhiliwa na USAID wa Tuhifadhi Maliasili unaoratibiwa na JET, lengo likiwa kuongeza uelewa kuhusu uhifadhi na ushirikishwaji wa wananchi kwa ujumla.

Kuhusu kuhamisha simba alisema hatua hiyo imetekelezwa hivi karibuni baada ya kutokea changamoto ya idadi ya wanyama kuongezeka kwa wingi katika eneo hilo.

"Manyara ranchi ni shamba linalojumuisha wanyamapori na mifugo kama ng’ombe na kutokana na kusimamiwa vyema wanyama wameongezeka na wanakuja eneo hilo kwa wingi," alisema Ole Kashe na kuongeza kuwa kutokana na simba kuua, wananchi nao walianza kujihami wakitaka kuua.


Aidha, alisema jamii ilipata shida kutokana na wanyamapori hao kuvamia mifugo katika vijiji viwili vinavyosimamiwa na shamba hilo ambavyo ni Esilalei na Ortukai wakiendesha shughuli za ufugaji pamoja na hifadhi ya ushoroba wa wanyamapori.

Kuhusu mnada alisema hivi sasa shamba hilo lina ng'ombe 980 na baada ya mnada walitaka zibakie 740 ili waweze kukabiliana nazo kulingana na hali ya kukosekana kwa malisho kutokana na ukame.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad