Sistiinho: Nimemuelewa Sana Sheria Ngowi kwenye Ubunifu Wake wa Jezi za Yanga



 

Sistiinho mchambuzi wa soka
MCHAMBUZI wa soka kupitia kipindi cha Krosi Dongo kinachorushwa na Studio za Global TV na 255 Global Radio Sistiinho, ameoneshwa kuridhishwa na ubora wa jezi mpya za klabu ya Yanga zilizozinduliwa rasmi jana.

Akiongelea ubunifu na ubora wa Jezi hizo mchambuzi huyo amebainisha kuwa Mbunifu wa jezi hizo Sheria Ngowi anapaswa kupongezwa sana kutokana na kuja na mawazo matatu taofauti ambayo yaetumika katika jezi zote tofauti za mashindano za klabu hiyo kwa msimu ujao.


Jezi ya tatu ya klabu ya Yanga
“Yes nilimuelewa ana Sheria Ngowi kwenye Home Kit ile, jezi ile ya kijani ameonesha vitu tofauti tofauti ameonesha vile vivutio na zile Iconic Monament ambazo zinapatikana sehemu tofauti tofauti kwenye nchi yetu, kuna mambo mengikwenye ile jezi ambayo inaonesha ni vivutio ambapo Yanga inaenda kimataifa ina maana vile vitu ni sehemu ya Royal Tour.” Amesema Sistiinho.


Jezi za nyumbani za Yanga
Klabu ya Yanga imezindua rasmi jezi zake hizo kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/2023 ambapo jezi yake ya kijani ni jezi ya mechi za nyumani na jezi ya njano ni kwa ajili ya mechi za ugenini huku jezi nyeusi ikiwa ni jezi namba tatu.


 

Jezi za ugenini za Yanga
Tayari jezi hizo zimeanza kuuzwa kwa mashabiki na wapenzi wa soka nchini katika maeneno mbalimbali nchini huku bei yake ikitajwa kuwa ni kiasi cha shilingi 35000/= kwa jezi moja.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad