Sitta, Ndugai walivyopandisha kushusha demokrasia bungeni



Dodoma. Bunge ni chombo muhimu katika kuonyesha demokrasia kwa vitendo nchini Tanzania, taasisi hiyo imekuwa na mchango wake katika mazuri na mabaya ndani ya miaka 30 ya siasa za vyama vingi.

 Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 1992 yaliondoa hadhi ya Bunge kuwa Kamati ya chama tawala ( CCM) na yakaanzisha haki za kikatiba za chombo hicho kuwa muhimili wa nchi.

Cheche za wapinzani

Wabunge wa upinzani waliingia bungeni baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 na kusaidia kushinikiza Bunge la Agosti kutekeleza majukumu muhimu ya kikatiba ya kuwa msimamizi wa Serikali. Baadhi ya wabunge waliohusika ni pamoja na Dk Masumbuko Lamwai aliyekuwa mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Mabere Marando (Rorya, NCCR-Mageuzi), James Mbatia (Vunjo, NCCR-Mageuzi) na Ndimara Tegambwage (Muleba kaskazini, NCCR-Mageuzi).

Baadaye mwaka 1996, Augustine Mrema, aliyeshinda ubunge wa Temeke kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mdogo, akaingia bungeni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad