M/kiti wa harusi ya @billnass na @officialnandy , @stevenyerere2 amedai anataniwa na taifa zima na sio @mwijaku pekee hivyo hicho kitu hakimsumbui, Tivu ake pia amedai yeye sio M/kiti bali ni Chairman of Wedding na anaenda kuionyesha Tanzania ni namna gani hiyo siku itaacha alama kwenye taifa hili, pia amedai amepokea simu za Mawaziri 7, Wabunge 14 na MaDC wasio na idadi wakitaka kuhudhuria Wedding.
Mbali na Hilo Chairman amedai Vyombo vyote vya habari nchini vitaonyesha harusi hiyo, lakini pia amepokea simu kutoka Al Jazeera wakitaka wairushe hewani Wedding hii😁. Kabla ya Wedding, Chairman amedai kutakuwa na sherehe zinazo itwa Bachelor Boy Party na Example Wedding Party, huku akithibitisha kuziandikia barua mamlaka, siku hiyo ya Wedding iwe ni Holiday, watu wasiende makazini.
Steve Nyerere amefunguka haya kupitia Leo Tena ya Clouds Fm hii leo July 05.