Mwenyekiti wa Kamati ya Harusi ya Billnass na Nandy, Steve Nyerere amesema harusi ya wawili hao itarushwa na karibia vyombo vyote vya habari nchini.
Steve Nyerere akiongea leo Jumanne, kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, amesema hadi CNN wameomba kurusha harusi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wengi.
Pia amebainisha kutakuwa na party ya siku tatu mfululizo kuelekea kwenye harusi hiyo. Steve amesema kesho atakuwa na press Serena Hotel ambapo atazungumza kwa mapana zaidi.
Ikumbukwe, ndoa ya Billnass na Nandy inatarajiwa kufungwa Julai hii.
Neno moja kwa M/Kiti 🤔