Web

TAARIFA :Upasuaji wa Kutenganisha Watoto Waliokuwa Wameungana Umefanyika kwa Mafanikio


Upasuaji wa kuwatenganisha Watoto waliokuwa wameungana (Neema na Rehema) umefanyika kwa mafanikio katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo Jopo la Wataalamu 31 wametumia saa saba kukamilisha upasuaji huo.

Watoto hao mapacha wawili wenye umri wa miezi tisa walizaliwa wakiwa wameungana sehemu ya kifua na tumbo na kwa upande wa umbo la ndani wameungana ini ila kila Mtoto ana ini lake.

Tanzania inakuwa nchi ya tatu Barani Afrika kufanya upasuaji wa aina hii baada ya Afrika ya Kusini na Misri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad