Takwimu mpya za UNAIDS zinaonesha kuwa kila dakika alifariki Mtu mmoja kutokana na ugonjwa unaohusiana na UKIMWI mnamo 2021, pia inakadiria kuwa kila dakika mbili mwaka 2021, Msichana au Mwanamke kijana alikuwa ameambukizwa HIV.
Ripoti hiyo -iliyopewa jina la In Danger - ilitolewa katika wa mwaka huu wa Global UNAIDS huko Montreal, Canada.
Ulimwenguni, Wanawake na Wasichana walichangia asilimia 49 ya maambukizi mapya mwaka 2021, hata hivyo, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, walichangia asilimia 63 ya maambukizi mapya katika mwaka huo huo.
Takribani Watu 1.5 waliambukizwa HIV mwaka jana kulingana na data, ripoti hiyo inaonesha zaidi kwamba maambukizi mapya yanaongezeka ambapo hapo awali yamekuwa yakipungua.
"Takwimu zilizofichuliwa katika ripoti hii zitasumbua na kushtua lakini ripoti hiyo sio sababu ya kukata tamaa, ni wito wa kuchukua hatua, kushindwa kunaweza kuwa kubaya lakini sio kuepukika, tunaweza kukomesha UKIMWI ifikapo 2030”