Uchaguzi Mkuu Kenya: Raila Odinga Asusia Mdahalo

 


Mmoja wa wagombea wa urais nchini Kenya, Raila Odinga hatashiriki kwenye mdahalo ujao kuhusu uchaguzi, timu yake ya kampeni imesema Jumapili, akimshtumu mpinzani wake mkuu kujaribu kukwepa baadhi ya mada nyeti kama vile ufisadi.


Odinga, mwenye umri wa miaka 77 na makamu rais William Ruto mwenye umri wa miaka 55, ndio wagombea wakuu kwenye uchaguzi wa rais wa Agosti 9.


Lakini katika taarifa inayoeleza kuwa Odinga atasusia mdahalo wa Jumanne, msemaji wa kampeni yake, Makau Mutua, amemshtumu Ruto kujaribu kukwepa mjadala wa masuala muhimu.


Ruto “aliomba mdahalo usijikite kwenye ufisadi, uadilifu, maadili na utawala, masuala muhimu ambayo Kenya inakabiliwa nayo,” msemaji wa Odinga amesema katika taarifa.


“Mdahalo wowote usio na masuala haya utakuwa tusi kwa akili ya Wakenya. Ndio maana hatuna nia ya kushiriki jukwa la kitaifa na mtu ambaye hana adabu ya kimsingi,” ameongeza.


Badala yake, Odinga anapanga kushiriki kikao kwenye ukumbi na Wakenya wa kawaida kitakachopeperushwa kwenye televisheni katika kitongoji cha mashariki mwa mji mkuu Nairobi, kulingana na taarifa ya msemaji wake.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad