Uchaguzi Yanga wanachama mapema tu, Mwigulu atinga



 
WANACHAMA wa klabu ya Yanga wamejitokeza kwa wingi kuandika historia nyingine ya viongozi wapya watakaoiongoza timu hiyo baada ya mabadiliko ya kiuendeshaji.

Yanga imefuata nyayo za watani zao Simba ambao waliingia katika mfumo huo licha ya kutokamalika mpaka sasa baada ya kukwama katika tume ya ushindani wa kibiashara (FCC).

Leo Julai 9 wanayanga wanaitumia siku hii kikatiba kuchagua viongozi wao Rais wa klabu Hersi Said ambaye yuko peke yake katika nafasi hiyo, Makam Mwenyekiti nafasi inayowaniwa na wagombea wawili Suma Mwaitenda na Arafat Haji.

Huku nafasi ya ujumbe wakitakiwa watano katika 17 wanaogombea nafasi hiyo.
Wakati huo huo wanachana wa Yanga wamejitokeza kuanzia saa 12 asubuhi wakisubiri kuanza kujiandikisha tayari kwa zoezi hilo.
Mpaka muda huu wanachama bado wamepanga mistari huku wengine wakiwa wameishaingia ndani.

Mwigulu naye ndani

WAZIRI wa fedha Mwigulu Nchemba amesema mambo safi ndio maana amelazimika kuja kujumuika na wanayanga kufanya uchaguzi.

Mwigulu amewasili katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo uchaguzi huo unafanyika leo akiambatana na mwanao wa kiume aliyevalia jezi ya Yanga.
Mwanaspoti imepata nafasi ya kuzungumzia machache na Mwigulu licha ya kuzongwa na wanayanga waliokuwa wakimuongoza kuingia ukumbini.
Mwigulu amesema "mambo safi mwandishi ndio maana nimekuja hapa namimi, kila kitu kitakwenda sawa," amesema kwa ufupi na kuingia ndani.


 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad